Baraka FM

Tamasha la Maryprisca mama ntilie festival 2023 lawapa kicheko mama lishe Busokelo Mbeya

6 October 2023, 12:04

Baadhi ya mama lishe wakifurahia baada ya kupewa mitungi ya gesi Busokelo Mbeya (picha na mwandishi wetu)

Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mmoja,wakati Dunia ikisisitiza kuachana na matumizi ya kuni na mkaa badala yake utumie teknolojia ya nishati gesi jamii inawajibu wa kutekeleza hayo ili kuepukana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Na mwandishi wetu

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameendelea na kampeni ya kuwawezesha wanawake kiuchumi Halmashauuri ya Busokelo bila kujali itikadi zao kwa kutoa majiko na mitungi ya gesi aina ya ORYX likiwa ni tamasha la pili baada ya lile la ufunguzi lilozinduliwa Tukuyu Jimbo la Rungwe.

Mbunge wa viti maalum Mbeya na naibu waziri wa maji Maryprisca Mahundi akiimkabidhi mama ntilie mfuko wenye unga (picha na mwandishi wetu)

Washindi watano wamepatiwa mtaji wa shilingi elfu thelathini ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa mafunzo chuo cha VETA Mbeya ili kuboresha kiwango ili biashara ifanyike kwa ufanisi zaidi.

Tamasha litaendelea Wilaya ya Kyela na washindi wa kwanza katika halmashauri zote watanufaika na mafunzo yatakayotolewa VETA.

mhe.Maryprisca Mahundi akifurahia jambo wakati akiwezesha mahitaji kwa mama lishe kwenye biashara zao(picha na mwandishi wetu)

Hata hivyo Mahundi ametoa majiko 21 ya ziada kwa wanawake waliotoka mbali ingawa hawakupata fursa ya kushiriki tamasha.