Baraka FM

Mbeya yazindua huduma ya utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto

21 September 2023, 15:47

Mmoja ya watoto walioshiriki katika zoezi la chanjo ya polio Iyela jijini Mbeya

Mkoa wa Mbeya ni moja ya mkoa wa Nyanda za Juu Kusini ambao umeanza leo zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto wenye umri wa miaka nane hii ni kutokana na uwepo wa mkoa wa katavi kuwa na kisa cha mgonjwa mmoja wa ugonjwa huo.

Na Sadock Mwaigaga

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amewataka wananchi kuhakikisha wanawapatia watoto wao chanjo ya polio ili kuwakinga na ugonjwa wa polio.

Mkuu wa mkoa Homera amesema hayo wakati akizindua utoaji wa chanjo ya matone ya polio katika kata ya Iyela ambayo itafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia septemba, 21 hadi septemba 24 mwaka huu.

Homera amesema chanjo hiyo haina madhara kwa watoto na wamejipanga kufika kila eneo kutoa huduma hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera akizindua chanjo ya Polio Iyela jijini Mbeya(Picha na Sadock Mwaigaga)
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera

Kwa upande wao madaktari waliohudhuria katika uzinduzi huo wamesema chanjo hiyo ni ya muhimu kwa kila mtoto kujikinga dhidi ya ugonjwa polio unaoweza kusababisha mtoto kupooza na watahakikisha kila mtoto anapata chanjo hiyo.

Sauti za baadhi ya madaktari walioshiriki katika uzinduzi wa chanjo ya polio Iyela jijini Mbeya

Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wameipongeza serikali kwa kutoa chanjo hiyo kwa watoto na wa namewaomba wahudumu wa afya kupita katika shule za watoto mbalimbali ili wapatiwe chanjo hiyo.

Mstahiki meya wa jiji la Mbeya Dormohamed Issa akishiriki zoezi la uzinduzi wa chanjo ya polio Iyela jijini Mbeya(Picha na Sadock Mwaigaga)
Sauti ya baadhi ya wananchi jijini