Baraka FM

Vyombo vya habari mbalimbali Nchini vyapatiwa mafunzo namna ya kutumia mtandao ya kijamii

7 March 2024, 13:15

Baadhi ya wataalamu wa It wakifuatilia mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa hotel ya Jamilex jijini Dar es salaam (picha na Hobokela Lwinga)

Mtandao wa rediotadio umekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo miongoni mwa radio ambazo wamekuwa wakifanya nao kazi.

Na Hobokela Lwinga

Radio tadio imeendesha mafunzo mafunzo kwa wataalamu wa It kutoka vyombo mbalimbali vya habari Nchini lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa matumizi mitandao ya kijamii katika kujipatia masoko.

Miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo ni kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Zanzibar na yanafanyika katika hotel ya Jamilex jijini Dar es salaam.

Mwalimu mafunzo Amua Rushita akiendelea kufundisha washiriki wa mafunzo katika ukumbi wa hotel ya Jamilex jijini Dar es salaam (picha na Hobokela Lwinga)

Wakati akifundisha mhariri wa radio tadio Hilali Ruhundwa amesema katika kuweka taarifa kwenye mtandao wa radio tadio inapaswa kufuata mlolongo sawa uliwekwa kumuwezesha msomaji kuvutiwa na habari hiyo.

Mhariri wa radio tadio Hilali Ruhundwa akiendelea kufundisha (picha na Hobokela Lwinga)

Aidha katika mafunzo hayo washiriki wameeleza mafanikio waliyoyapata tangu kujiunga na mtandao wa rediotadio ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa wasikilizaji sambamba na kupata masoko kwa wateja wapya.

Semina hiyo imeanza march 7 inatarajiwa kuhitimishwa March 8 mwaka 2024.