Baraka FM

Homera aongoza kikao kamati ya ushauri mkoa wa Mbeya

22 February 2024, 20:42

Na Mwandishi wetu

Leo February 22, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z Homera ameongoza Kikao Cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya(RCC) kilicholenga kujadili, kushauri na Kutoa Mapendekezo juu ya Namna bora ya kutatua baadhi ya Changamoto zinazoukumba Mkoa.

Wajumbe wa Kikao hicho wakapata Nafasi na fursa ya kujadili Mambo kadha wa kadha ikiwemo mfumuko wa Bei ya Sukari, Uboreshwaji wa huduma za Afya, Barabara na Miundombinu mingine.

Kikao Cha RCC kimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z Homera akiwa M/kit wa Kikao na Kuhudhuliwa na Wajumbe Mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt: Tulia Ackson Chama Cha Mapinduzi Mkoa kadharika Wabunge wa Mkoa wa Mbeya na wataalam Mbalimbali.