Baraka FM

Askofu Mteule Moravian KMT-JKM awataka waumini kuacha makundi

6 November 2023, 15:09

Ni siku tano tu zimepita kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi limefanya uchaguzi wa kumpata askofu,na katika uchaguzi huo mchungaji robart pangani ndiye ambaye alichaguliwa katika nafasi hiyo.

Na Hobokela Lwinga

Askofu mteule na mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani amewataka waumini kuondokana na makundi mbalimbali kwenye kanisa badala yake kila mmoja anapaswa kusimama kufanya kazi ya Mungu kwa zamu yake.

wito huo ameutoa katika ibada yake ya Kwanza jumapili katika ushirika wa jakaranda jijini Mbeya tangu kuchaguliwa kwake na mkutano wa sinodi November 2 mwaka huu 2023.

Askofu mteule na mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Askofu mteule na mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani

Askofu huyo Amesema kabla ya kupewa nafasi ya kuongoza katika nafasi ya uaskofu amesema alishawahi kuambiwa na marehemu mama yohana wavenza enzi za uhai wake kwamba ajiandae kushika wadhifa huo.

Aidha mch.Pangani amesema amekubali wito huo na yuko tayari kuliongoza kanisa huku akiomba ushirikiano pamoja na kila mwamini wa kristo kuendelea kuliombea kanisa.

sauti ya Askofu mteule na mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani

Askofu mteule mchungaji Robert Pangani anakuwa Askofu wa tatu katika Jimbo la kusini magharibi akitanguliwa na Askofu Yohana Wavenza na Askofu Alinikisa Cheyo.

baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Jakaranda jijini Mbeya(picha na Hobokela Lwinga)