Baraka FM

Mbunge Mwantona akabidhi mifuko 50 ya saruji shule ya msingi Kibwe

11 April 2024, 19:54

Baadhi ya wananchi wakata ya Iponjola wakishusha mifuko ya saluji(picha na Ezra Mwilwa)

Baada ya uchakavu wa miundombinu katika shule ya msingi Kibwe Mbunge Mwantona ametoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya

Na Ezra Mwilwa

Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mhe Anton Mwantona leo Amekabidhi mifuko 50 ya saruji kata ya iponjola shule ya msingi  kibwe kwa ajili ya ujenzi wa Darasa la Awali na Ofisi ya walimu

Katibu wa Mbunge Mwantona akipongeswa na mwananchi wa kata ya Iponjola(picha na Ezra Mwilwa)

Sambamba na mifuko hiyo ya saruji ameahidi kuwaongezea mifuko 50 ili itimie mifuko miamoja pindi tu watakapomaliza mifuko aliyopeleka.

auti ya katibu wa Mbunge Mwantona

Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibwe Furaha Joshua amemshukuru mbunge huyo na kuwaomba wananchi wa kata ya Iponjola kuendelea kumuunga mkono Mbunge huyo.

Katibu wa Mbunge Mwantona na Mwalimu Furaha Joshua(katikati wakipeana mkono wa pongezi)picha na(Ezra Mwilwa)
Sauti ya Mwalimu Furaha Joshua