Baraka FM
Baraka FM
18 April 2026, 01:08

Kanisa la Moravian limekuwa na utaratibu wa kuwajengea uwezo watendaji wake katika idara mbalimbali za kanisa hilo.
Na Hobokela Lwinga
Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Robert Pangani amefungua semina ya idara mipango uchumi na maendeleo ya jimbo hilo inayofanyika katika kanisa la Moravian ushirika wa Itili.
Semina hiyo imeandaliwa na Idara hiyo ikiwa imefadhiliwa na shirika la mission 21 na imehusisha viongozi wa Idara hiyo kutoka katika shirika zote za kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi.
katika ufunguzi huo Askofu Pangani Amewataka washiriki hao kuishi maisha ya kumtegemea Mungu kwani kazi waliyoitiwa inahitaji Nguvu za Mungu sambamba na kufanya kazi hiyo kwa weledi.

Hata hivyo Makamu mwenyekiti KMT-JKM mchungaji Agnes Njeyo amesema utekelezaji wa mpango mkakati wa Jimbo unahusisha viongozi wote kuanzia ngazi ya ushirika walichaguliwa kusimimia nafasi za uongozi wa kanisa kwa miaka mitano.

Mkufunzi Katika semina hiyo Solomoni kibona kutoka ushirika wa Mabibo Jimbo la mashariki kanisa la Moravian amesema ili kufanikiwa kwenye shirika au maisha ya kila mtu ni lazima uwe na mipango sambamba na kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo yao.

kwa upande wake mkurugenzi wa mipango, uchumi na maendeleo KMT-JKM Esau Swila amezitaka wilaya kuandaa mpango kazi unaoendana na mpango kazi wa Jimbo.

Zaidi ya washiriki 150 kutoka Katika shirika zote zinazounda Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi wameshiriki semini hiyo.
