Baraka FM

Wadau waombwa kusaidia watoto wenye uhitaji

26 March 2024, 19:03

Baadhi ya watoto yatima kituo cha Amani Nsalaga(picha na Ezra Mwilwa).

Katika ulimwengu huu hakuna anayejua kesho yake hivi ndivyo unaweza kusema baada ya baadhi ya watoto kujikuta wapo kwenye mazingira magumu baada ya kupoteza wazazi.

Na Ezra Mwilwa

Wadau mbalimbali wameomba kujenga tabia ya kutembelea wahitaji mbalimbali na watoto yatima kwa kuwapatia Mahitaji yatakayowaondolea changamoto zinazowakabili.

wito huo umetolewa na mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima na mahitaji maalumu cha Amani nsalaga kilicho chini ya kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi Mch. Elizabeth Nampasa Wakati akiwapokea wadau mbalimbali walifika kuwaona wahitaji hao.

Sauti ya Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima na mahitaji maarumu Amani Nsalaga

Mch. Nampasa ameongeza kuwa kama kituo wanamradi wa shamba la palachichi Mkoa wa Njombe hivyo wanaomba wadau kuwaunga mkono kwaajili ya kuuendeleza mradi huo.

Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima na wenye mahitaji Maalumu Mch. Elizabeth Nampasa(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Mchungaji Elizabeth Nampasa akiwaomba wadau kuwaunga mkono

Nao baadhi ya wadau walio fika katika kituo hicho kutoka maeneo mbalimbali wamesema ni vizuri kutengeneza tabia ya kutembelea wahitaji mbalimbali.

Wadau mbalimbali wakiwa nawatoto waliopo kituo cha Amani Nsalaga (picha Ezra Mwilwa)
Sauti za wadau walio fika katika kituo hicho kuwaona watoto hao

Nao baadhi ya watoto walio patiwa msaada huo wametoa shukrani zao na kuahidi kuendelea kuwaombea watu wanaofika kituoni hapo.

Baadhi ya watoto wakipokea zawadi za Daftari (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti za baadhi ya watoto wakitoa shukrani zao