Baraka FM

Mbeya kukaguliwa miradi ya maendeleo

23 November 2023, 18:27

Na Hobokela Lwinga

Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh.Juma Zuberi Homera anatarajia kuanza ziara katika halmashauri za Jiji la Mbeya na Mbeya Dc lengo likiwa ni kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Akitoa taarifa ya ziara hiyo kwa vyombo vya habari mkuu wa wilaya ya Mbeya mh.Beno Malisa amesema ziara hiyo itaanza November 24,hadi 30 mwaka huu.

Mhe.Malisa ameitaja baadhi ya miradi itakayotembelewa kuwa ni katika sekta ya elimu,afya sambamba na miundombinu ya barabara.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya mh.Beno Malisa (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mbeya mh.Beno Malisa

Mkuu wa mkoa Juma Zuberi Homera amekuwa na utaratibu wa kutembelea wilaya zake zote kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi.