Baraka FM

Askofu Mwakyokile aishukru halmashauri ya wilaya ya Rungwe

8 January 2024, 14:37

Na Hobokela Lwinga

Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe Jaffar Haniu; Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Konde Mchungaji Dkt Israel Mwakyolile ameishukuru Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo ambapo miradi mingi imetekelezwa na kukamilika kwa Viwango Stahiki.

Shukrani hizi amezitoa wakati Mhe.Haniu akizindua zahanati ya Ilenge iliyopo katika kata ya Kyimo.

Dkt Makyolile ambaye pia ni mkazi wa Ilenge amepongeza kwa hatua iliyofikiwa ya kuzinduliwa kwa zahanati hii na kuwa itasaidia kuboresha afya ya wakazi wa Kyimo (Ilenge) na kuwapunguzia Kutembelea umbali mrefu hasa Mama na Watoto.

Dkt.Mwakyolile ambaye pia ni mdau wa Michezo amesema serikali kwa muda mrefu imekuwa ikipeleka huduma za jamii kwa wananchi ikiwemo maji, elimu na afya hatua inayosaidia kuchochea maendeleo na ustawi wa jamii.