Baraka FM

TADIO yapongezwa, yaombwa kuongeza wigo zaidi elimu kwa wanahabari

18 September 2023, 19:14

Picha ya pamoja washiriki, mkufunzi na mratibu wa mafunzo.

Kila binadamu anapaswa kuwa na utu na binadamu asiyekuwa na utu hawezi kuona wema anaotendewa, unapofanyiwa jambo lenye utu unapaswa kuwa na shukrani na ndivyo ilivyo pia msisitizo katika vitabu vitakatifu vya dini.

Na Hobokela Lwinga

Wahariri na wakuu wa kidijitali waliopata mafunzo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wameishukuru taasisi ya maendeleo ya radio za jamii Tanzania TADIO kwa kutoa mafunzo ya radio mtandao ambayo kwao yamekuwa na tija ya kwenda kuongeza uchumi kwenye vyombo vyao.

Shukrani hizo wamezitoa baada ya kukamilika kwa mafunzo ya siku mbili katika ukumbi wa hotel ya Usungilo jijini Mbeya yakihusisha mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Njombe, Iringa na Ruvuma.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo
Sauti ya washiriki wa mafunzo

Afisa mradi na afisa habari kutoka TADIO Bi. Saum Bakari amesema matarajio makubwa ya TADIO ni kuona wanufaika wa mafunzo wanakwenda kutumia teknolojia ya radio mtandao. Ameomgeza kuwa mafunzo hayo ni endelevu hivyo wanajiandaa kwenda mikoa ya kaskazini ili nao waweze kunufaika.

Mratibu wa mafunzo kutoka TADIO Bi. Saum Bakari

Sauti ya mratibu wa mafunzo kutoka TADIO Saum Bakari.

Kwa upande wake mkufunzi kutoka TADIO Amua Rushita amesema ameona mwitikio wa washiriki kuvutiwa na mafunzo ya radio mtandao hivyo anaamini watakwenda kuonesha na kufanya mabadiliko makubwa ya kidijitali.

Baadhi ya washiriki wakiwa wanasikiliza mawasilisho ya wanavikundi kwenye mafunzo (picha na Hobokela Lwinga)

Sauti ya mkufunzi wa mafunzo Amua Rushita