Baraka FM

Watu kadhaa wahofiwa kufariki ajalini Mbeya

31 December 2023, 10:07

Na Kelvin Lameck

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika ajali iliyotokea mapema leo katika eneo la Mbembela kata ya Nzovwe jijini Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha magari matatu ikiwemo roli pamoja hiace mbili ambazo zilikuwa na abiria zikifanya safari zake Sokomatola Mbalizi.

Katika ripoti ya awali iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga amekiri kutokea kwa ajali hiyo, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi huku akisema chanzo cha ajali ni gari lori namba T428 DXD kufeli break kisha kugonga gari zingine tatu zikiwemo hiace mbili zinazofanya safari kati ya Mbalizi na Sokomatola zilizokuwa na abiria ndani yake.