Baraka FM
Baraka FM
3 March 2025, 10:08

Katika kuadhimisha kilele cha siku ya mwanamke Duniani wanawake mkoani Mbeya watumia nafasi hiyo kuwatembelea wahitaji mbalimbli.
Na Ezra Mwilwa
Kuelekea siku ya mwanamke duniani Umoja wa kina mama mtaa wa Block D Ilomba wametembelea gereza la Ruanda upande wa wanawake kwa lengo la kuwafariji na kuwapelelea baadhi ya mahitaji.
Makamu mwenyekiti wa umoja huo Neema Kibona amesema katika kuadhimisha siku ya mwanamke Duniani wamekua na utaratibu wa kutembelea wahitaji.

Kibona amewawaomba wanawake wote kunitumia siku hiyo kusaidia wahitaji waliopo maeneo tofautitofauti.
naye Askari Mkaguzi msaidizi Juliana Akioo kutoka gereza la Rwanda amewashukuru wanawake hao kwakutambua uhitaji wawanawake wafungwa gerezani.

Siku ya mwanamke Duniani imekua ikiadhimisha Kila mwaka ifikapo mwezi Machi tarehe 8