Baraka FM

Iponjola washiriki christmas kwa kuchimba shimo la maji  

28 December 2023, 17:59

Na Hobokela lwinga

Katika kuadhimisha sikukuu ya Krismas Mamia ya Wakazi wa kata ya Iponjola wilayani rungwe wameshiriki zoezi la Uchimbaji wa Shimo la maji taka katika kituo cha afya kilichopo katika kata yao.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni hatua ya uungaji mkono wa juhudi za Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo ameipatia kata hii shilingi Million 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Kituo kipo katika hatua ya ukamilishaji kikijumuisha jengo la mama na mtoto, Wagonjwa wa nje, Maabara, vyoo na jengo la kufulia.

Kituo hiki kilichopo karibu na shule ya Msingi Ilalabwe kijiji cha Ngana kinatajwa  kuondoa  changamoto ya wakazi wa kata hii na maeneo ya jirani kufuata huduma ya matibabu katika kata ya kyimo na Ikuti pamoja na Hospitali ya Wilaya Tukuyu Makandana.