Baraka FM

Rasmi chuo kikuu cha Kikatoliki Mbeya CUoM chapanda hadhi

16 January 2024, 18:39

Na Hobokela Lwinga

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa rasmi amekizindua na kukipandisha Hadhi chuo kikuu kishiriki Cha Cathoric University Collage of Mbeya (CUCoM) na kuwa chuo kikuu kamili Cha kikatoliki Mbeya (CUoM) Leo January 16 2024.

Awali akifungua chuo hicho kwa kusoma hotuba kabla ya zoezi la kukata utepe Mh Majaliwa amevitaka vyuo vikuu vyote nchini kutoa elimu inayomuwezesha muhitimu kujiajiri na kuendana na soko la ajira duniani.

Hata hivyo Ameutaka Uongozi wa Chuo hicho Cha CUoM kupitia Upya Watumishi wao na kutosita kuwapunguza hasa wale wasio na Uwezo wa kuendana na Kasi/hadhi ya Chuo Kikuu Lengo ikiwa ni kuendeleza Ushindani wa Kitaaluma kwa Vyuo vikuu vingine.