Baraka FM

Rungwe Mbeya yampokea mwenyekiti wa ccm mpya

19 December 2023, 19:49

Shangwe ya Mapokezi ya Mwenyekiti Mpya wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Patrick Mwalunenge Katika Wilaya ya Rungwe lmefana baada ya Mamia ya wakazi wa wilaya ya Rungwe kujitokeza Kumlaki.

Mapokezi yamefanyika katika uwanja wa stendi ya daladala Tukuyu mjini.

Mwalunge amechaguliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hiki  Mhe.Stephen Mwakajumilo  baada kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Dira ya Maendeleo ya taifa huakisi Ilani ya Chama kilichopata ushindi  katika Uchaguzi Mkuu na kuongoza dola ambapo CCM ndiyo chama Tawala nchini  Tanzania.

Hivyo Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imeendelea kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kujenga Vituo vya kutolea huduma ya elimu na afya, Barabara, Maji, Mikopo ya asilimia 10%, Umeme, Kilimo, Mifugo, Misitu na mengine mengi.