Baraka FM

Tumejiandaa vyema kumpokea Dr. Tulia

10 November 2023, 17:14

Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya mjini  Ndg Clemence Mwandemba  amempongeza  Rais wa JMT Dr Samia Suluhu Hassan  Kwa kuwa kiungo hatari mchezeshaji katika Ushindi wa Dr Tulia, pale Nchini Angola ,Dr Samia amepiga asist nyingi Pale IPU na Dr Tulia zote ameweka kambani , Ndio maana Dr Samia anakuwa mpiga Asisit  Bora wa Dunia.

Mwenyekiti ameyasema hayo alipokuwa akifunga mashindano ya Ndondo cup Mbeya, ambapo amewaasa vijana kuipenda nchi yeo kupitia michezo tuendelee kudumisha amani ambayo Rais wetu amekuwa akiihubiri Kila Siku ,

Mwandemba alitumia nafasi hiyo kugawa zawadi Kwa washindi ,na kuzipongeza team zote zilizoshiriki katika Mashindano  hayo

Tarehe 11/11/2023 Jumamosi Tuna mapokezi mazito ya Kumpokea Mama wa  Dunia  Rais wa Mabunge Dunia (IPU) ambaye ni Mbunge wetu na Spika wetu wa Bunge, Wanamichezo wote mnakaribishwa Sana na Mama yetu huyu  Uongozi wake unamchango Mkubwa katika kuinua michezo Kwa ujumla 

Mapema Sana , Tunampokea Mama  Jumamosi katika viwanja vya Ruanda nzovwe kuanzia saa mbili asubihi