Baraka FM
Baraka FM
3 March 2025, 09:22

Wanandoa mara zote huwa wanashauri kushirikiana pamoja katika maamuzi,hali hiyo imekuwa tofauti kwa ndoa za sasa.
Na Ezekiel Kamanga
Kijana George Arubati (29) mkazi wa mtaa wa Kanda ya Juu, kata ya Iduda jijini Mbeya amefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa sumu ya kukausha majani kwa kile kinachodaiwa kuwa mke wake ana madeni mengi katika vikundi mbalimbali.Baadhi ya majirani wanahisi chanzo cha kijana huyo kudaiwa kujiua ni kutokana mke wake kudaiwa fedha na vikundi mbalimbali bila mume wake kujua na alipotaka kujua aliambiwa madeni hayo hayamhusu pamoja na watu mbalimbali kuja nyumbani kwake kuulizia fedha zao.
Mke wa marehemu Zuhura Mussa amesema siku ya tukio februari 26,2025 alikwenda shambani lakini aliporejea akamkuta mume wake akiwa amelala na alipomuuliza kama ana shida akasema hana shida lakini baadaye akabaini kuwa amekunywa sumu ndipo alipoomba msaada na kusaidiwa kumfikisha hospitali lakini februari 28,2025 akafariki dunia.
Balozi wa shina namba sita katika mtaa wa Kanda ya Juu anayejulikana kwa jina la Jumanne Donald na Mwenyekiti wa Kanda ya Juu Maiko Mwanjalila wameeleza namna ambavyo wamesuluhisha ugomvi wa mume na mke huyo mara kadhaa kuhusiana na mume huyo kumlalamikia mke wake kukopa bila kumshirikisha.