Baraka FM

Wananchi wapigwa marufuku kuuza mazao kiholela

26 March 2024, 09:31

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba Mhe. Mathew Chikoti(picha na mwandishi wetu)

Akiba ni msingi wa maendeleo,Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa ya nyanda za juu kusini inayosifika katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara,kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kusahau kesho yao pale wanapovuna mazao na wanajikuta wanauza mazao yote ilihali wanatakiwa kula kesho.

Na mwandishi wetu, Songwe

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba Mhe. Mathew Chikoti Katika ziara yake ya kikazi iliyofanyika mnamo Tarehe 24 Machi, 2024. katika kata ya Kapele,Nkangamo,Myunga na Nzoka,

Amewaagiza Watendaji na wenyeviti wa kata hizo kuhakikisha wanatoa Elimu Kuelekea kipindi hiki cha mavuno, wananchi kutokuuza Mazao yao kiholela (Hovyo hovyo).

Aidha Chikoti amesisitiza utunzaji wa chakula kwa wananchi kuepukana na tatizo la njaa (ukosefu wa chakula ) kama iliyotokea miaka iliyo pita,
Hivyo na kuwataka wenyeviti na watendaji hao kuhakikisha kila kijiji kinatenga eneo maalumu la kuuzia mazao ili kuepusha ulaghai unaofanywa na baadhi ya wachukuzi wa mazao.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Momba ndg. Michael N. Nzunda naye amesema kuwa kwa kijiji kitakacho vuka lengo la ukusanyaji wa mapato yaliyopangwa na Halmashauri zidio lile litarejeshwa katika kijiji husika kwaajili ya kununua pikipiki ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato zaidi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Momba ndg. Michael N. Nzunda(picha na mwandishi wetu)

Mwishoni Mwenyekiti chikoti, amewapongeza watendaji na wenyeviti wa vijiji hivyo , kuwasisitiza kuwa mstari wa mbele katika ukusanyaji wa mapato kwani kupitia mapato hayo ndio chachu ya maendeleo ya vijiji vyao na Halmashauri kwa ujumla.