Baraka FM

Waumini wa dini watakiwa kuwasikiliza na kuwaheshimu viongozi wa serikali ngazi zote

11 October 2023, 10:52

Mch.Godfrey Tinga wa kanisa la Moravian ushirika wa chunya akizungumza na kituo hiki juu ya kuheshimu mamlaka za serikali (picha na Deus Mellah)

Kuwa muumini wa dini fulani hakuondoi wewe kujitenga na mamlaka za Dunia kwani katika Dunia kuna nchi na katika nchi zipo mamlaka ambazo zimewekwa ili kuongoza raia wake kwa mjibu wa katiba za nchi zao,hata vitabu vya dini vimekuwa na msisitizo wa waumini wao kuheshimu mamlaka za nchi zao kutokana na nje ya imani zao ni lazima waishi kulingana na miongozo ya utaratibu wa sheria.

Na Deus Mellah

Wakristo wa madhehebu mbalimbali nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafanya kazi mbalimbali zinazotangazwa na viongozi wao wa serikali kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya juu.

Wito huo umetolewa na Mch. Godfrey Tinga wa kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi ushirika wa Chunya mjini wakati akizungumza na kituo hiki kuhusu umuhimu wa Wakristo kutii mamlaka zinazowaongoza.

Mch. Tinga amesema ili Mkristo aweze kuishi vizuri ni vema akawa mstari wa mbele kutii mamlaka inayomuongoza.

Nao baadhi ya waumini jijini Mbeya wamesema baadhi ya Wakristo wamekuwa waoga kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazojitokeza serikalini hali inayosababisha kushindwa kutimiza wajibu wao.