Baraka FM

Mwl Luvanda: Utalii wa ndani unavutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi

30 October 2023, 17:14

Mwonekano wa Ziwa Nyasa majira ya jioni (picha na Josea Sinkala)

Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali ikiwemo hifadhi za wanyama,fukwe za maziwa na bahari pamoja malikale.

Na Josea Sinkala.

Kampuni ya Mwalimu Edwin Luvanda ya jijini Mbeya (Mc Luvanda Branding and Entertainment Company Limited) imehamasisha jamii kufanya utalii wa kutembelea fukwe za ziwa Nyasa na vivutio mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Mbeya ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza wilayani Kyela, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mwl. Edwin Luvanda ambaye pia ni mshereheshaji amesema kupitia kundi la WhatsApp analolisimamia la Usiku wa Maharusi wamekuwa wakiandaa matukio mbalimbali kwa mwaka wa nne sasa ili kuhamasisha utalii katika maeneo mbalimbali nchini hasa mkoani Mbeya.

Mwalimu Luvanda amesema serikali inajitahidi kutangaza Utalii lakini baadhi ya watu katika jamii hawana mwamko wa kwenda kutembelea vivutio na kupata muda wa kupumzika ili kupumzisha akili zao.

Amesema pia inasaidia watu hasa wanandoa kupata muda wa kupumzika ili kutengeneza familia zao ili ziendelee kukua katika furaha na upendo.

Mkurugenzi wa Mc Luvanda Branding and Entertaiment Company Limited Mwl. Edwin Luvanda(picha na Josea Sinkala)
Sauti ya Mkurugenzi wa Mc Luvanda Blanding and Entertaiment Company Limited mwl.Edwin Luvanda

Yuster Mbalaswa ni Mwalimu kutoka Shule ya watoto Shekinah Day care amesema waliamua kuwa moja kati ya wadhamini wa utalii huo wa ndani kwakuwa wazazi na walezi wanapokuwa na upendo, amani na mshkamano ndio chanzo cha kupata watoto watakaojengewa msingi imara kupitia elimu.

baadhi ya vifaa vinavyotumika kutoa burudani ziwa nyasa boti (Mbele) na mtumbwi(nyuma)(picha na Josea Sinkala)
Sauti ya Yuster Mbalaswa ni Mwalimu kutoka Shule ya watoto Shekinah Day care

Washiriki mbalimbali na wananchi wameeleza kufurahishwa na utalii huo na kuahidi kuwa mawakala kwa wenzao kuwahimiza kuwa na desturi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kwa faida yao kiafya na kukuza uchumi wa nchi.

baadhi ya washiriki katika safari ya utalii iliyoandaliwa na Mc Luvanda Blanding and Entertaiment Company Limited(picha na Josea Sinkala)
Sauti za washiriki