Baraka FM

Wananchi wajenga shule ya sekondari, serikali yatia mkono

16 January 2024, 10:19

Na mwandishi wetu

Isaka sekondari, shule mpya katika kata ya Nkunga ambayo imesajiliwa kwa namba S. 6491 na tayari imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Kuanzishwa kwa shule hii kumesaidia kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani katika shule ya sekondari Nkunga sambamba na changamoto ya kutembea umbali wa zaidi ya Km 05 kufuata huduma ya elimu.

Shule imejengwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri, Serikali kuu pamoja na nguvu za wananchi kutoka katika kata hiyo.