Baraka FM

Msyaliha: Wahitimu theolojia tumieni elimu yenu kuhubiri injili

10 October 2025, 18:44

Baadhi ya wahitimu chuo cha Theolojia Utengule(picha na Kelvin Lameck)

Watumishi mbalimbali wanao pata masomo ya theolojia watakiwa kumtumikia Mungu kutokana na elimu wanayo ipata.

Na Kelvin Lameck

Wahitimu wa masomo ya theolojia katika chuo cha biblia Utengule kinachomilikiwa na kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi wametakiwa kutumia elimu waliyoipata chuoni hapo kuhakikisha wanaeneza injili ya kweli kwenye jamii.

Hayo yameelezwa na kaimu katibu mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Nsevilwe Msyaliha wakati akiwa katika mahafali ya 18 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 10 Oct 2025.

Mch Nsevilwe Msyaliha(picha na Kelvin Lameck)

Aidha Mch. Nsevilwe amesema kwa wahitimu ambao wamebaki chuoni wanatakiwa kuendelea kusoma kwa bidii ili watakapohitimu masomo Yao waende kufanya kazi waliyohitiwa.

Naye Mchungaji Ryson Kibona ambaye ni Makamu Mwenyekiti Kanisa la Moravian Jimbo la Mbozi amewapongeza wahitimu hao na kuwataka kuwa mfano kwenye jamii kwa kutenda mambo mema.

Mchungaji Ryson Kibona(picha na Kelvin Lameck)

Akitoa mahubiri katika mahafali hayo Mch. Amosi Mwampamba amewataka wahitimu wote kushikamana ili kuhakikisha kanisa linapiga hatua katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi na kuongeza miradi.

Akitoa salamu za serikali katibu wa Baraza la kata ya Utengule Usongwe Benald Mgala amewaomba wahitimu kwenda kuhubiri amani sambamba na kuhimiza wananchi kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba 29,2025.

Mch Msyaliha akikabidhi cheti(picha na Kelvin Lameck)

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu Staford Mwaitenda ameshukuru uongozi wa chuo na walimu kwa namna walivyojitoa kufundisha na kuhakikisha wanaenda kuwa viongozi Bora katika maeneo mbalimbali watakayotumika sambamba na kutaka mafanikio mbalimbali.