Baraka FM

Mch. Sanga asimikwa mwenyekiti Moravian dinari ya Iwambi

5 May 2026, 20:57

Mwenyekiti wa Wilaya ya Mbeya Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Mchungaji Greenwell Sinkwembe (aliyesimama)akitoa mbaraka kwa mch.Fadhili Sanga na mke wake

Makanisa Mengi ya yaliyo chini ya jumuiya ya kikristo Tanzania CCT yanao utaratibu wa kuwasimikia watendaji wake wa kanisa pindi wanapata nafasi ya uongozi.

‎Na Hobokela Lwinga

Mwenyekiti wa Wilaya ya Mbeya wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Mchungaji Greenwell Sinkwembe, amemsimika rasmi Mchungaji Fadhili Sanga kuwa Mwenyekiti wa Dinari ya Iwambi.

‎Ibada ya kumsimika Mchungaji Sanga imefanyika jumapili mei 03,2026 katika Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi, Ushirika wa Iwambi jijini Mbeya, ambapo waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa walihudhuria.

‎Miongoni mwa wageni waliohudhuria ibada hiyo ni Katibu wa Wilaya ya Mbeya, Mchungaji Yasinta Sanga, pamoja na wachungaji kutoka shirika mbalimbali zinazounda Dinari hiyo.

Ndani ya ibada mchungaji Fadhili Sanga akiwa na mke wake.

‎‎Aidha, waumini kutoka shirika tofauti walishiriki kwa wingi katika ibada hiyo, wakishuhudia tukio hilo muhimu la kumsimika kiongozi mpya wa Dinari ya Iwambi.

Viongozi wa wilaya katika picha ya pamoja na viongozi wa Dinari ya Iwambi