Baraka FM

Rungwe waandaa bajeti ya mwaka 2024/25

28 December 2023, 18:00

Na mwandishi wetu

Maandalizi ya Bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa mwaka wa fedha 2024/25 yameendelea katika ukumbi wa kituo cha Kilimo Ilenge kata ya Kyimo.

Pamoja na mambo mengine Watalamu wameendelea kuchakata vipaumbele vitakavyosaidia kuleta maendeleo endelevu kwa wakazi wa wilaya ya  Rungwe Rungwe District Council .

Bajeti ndiyo mhimili na uti wa mgongo wa maendeleo ya nchi na maandalizi yake huanza kwa hatua ya ushirikishwaji wa wananchi kuibua vipaumbele vyao ngazi ya kijiji na kisha huviwasilisha katika kamati ya maendeleo ya kata (KAMAKA) ambapo hujadiliwa na kuvipeleka katika ofisi ya  Mkurugenzi (Halmashauri).

Hatua nyingine ni watalamu wa Halmashauri kujadili vipaumbele  kwa kina na kisha huingia katika Menejimenti ya Halmashauri ((CMT), Kamati ya Fedha (FUM), Baraza Maalumu la Bajeti na hatimaye rasimu yake hupelekwa Bungeni kwa ajili ya Mjadala zaidi.