Baraka FM

Zaidi ya wakulima 1326  na maafisa ugani 20 wamepatiwa elimu kilimo bora

15 November 2023, 17:51

Na Ivillah Mgala

Zaidi ya wakulima 1326  na maafisa ugani 20 kupatiwa elimu na mafunzo ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya mbarali mkoani Mbeya.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya mbarali mkoani Mbeya Kanali Denis Mwila katika hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya watu wa marekani USAID ya kuwasaidia wakulima wa mbogamboga na matunda iliyofanyika katika kijiji cha mapunga kata ya igurusi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema pamoja na hayo pia yapo mashamba darasa 21 yameanzishwa lengo likiwa ni kuwafundisha Kwa vitendo wakulima Ili waweze kulima Kwa tija.

Mkuu wa wilaya ya mbarali mkoani Mbeya Kanali Denis Mwila(picha na Ivilla Mgala)
Sauti ya mkuu wa wilaya ya mbarali mkoani Mbeya Kanali Denis Mwila

Kwa upande  wake mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kilimo Tija  Antonio Coello amesema zaidi ya bilioni nne zimekopeshwa Kwa wakulima wa mboga mboga na matunda katika halmashauri 19 nchini zinazofanya kazi na mradi huo unaofadhiliwa na USAID.

Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kilimo Tija  Antonio Coello
Sauti ya mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kilimo Tija  Antonio Coello

Naye mkulima wa mfano wilaya ya mbarali Fanuel  Vahaye amesema wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi kuliko faida ikiwemo ukosefu wa soko,ucheleweshwaji wa pembejeo pamoja kutokuaminiwa na taasisi za kifedha.

Mkulima wa mfano wilaya ya mbarali Fanuel  Vahaye
Sauti ya mkulima wa mfano wilaya ya mbarali Fanuel  Vahaye