Baraka FM

Viongozi idara za Moravian zapewa elimu kupinga ukatili

2 May 2024, 11:58

Utaratibu wa kanisa Moravian Ni kuhakikisha idara zake zinakuwa sehemu ya kuungana na jamii kupinga masuala ya ukatili yanayofanywa kwenye jamii.

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini kupitia Idara yake ya Ustawi wa jamii Inaendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo waelimisha rika kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Jimbo hili.

Mafunzo haya yaliyoanza 1/05/2024 yanaendelea leo hapa ndani ya ukumbi wa Moravian Hostel Tukuyu, na yanatarajia kuweka tamati siku ya Ijumaa 3/05/2024.

Akizungumza Katibu wa Idara ya Ustawi wa jamii Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Mch. Lillian Emanuel amesema tunawaanda na kuwapika waelimisha rika ili wawe na elimu ya kutosha ya mambo mbalimbali yanayojitokeza kwenye jamii ikiwemo mambo ya Afya pamoja na Ukatili wa kijinsia.

Semina hii inayofadhiliwa na Shirika la Mission 21, imekuwa muendelezo tangu 2020 ambapo jamii imeendelea kunufaika kupitia ufadhili huu.