Baraka FM

Viongozi wa dini waja na mkakati kabambe kilimo cha ufuta

25 April 2024, 21:39

Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika semina iliyowakutanisha viongozi wa makanisa yote Tanzania (Picha na Ezra Mwilwa)

Kwa kutambua umuhimu wa kilimo nchini, taasisi za dini zimejikita katika uzalishaji wa mazoa biashara katika kilimo cha ufuta.

Na Ezra Mwilwa

Umoja wa Makanisa Tanzania umejipanga kuanzisha mradi wa kilimo cha ufuta ili kuinua uchumi wa nchi. Kauli hiyo imetolewa na Askofu Prof. Silivesta Gamanywa wakati akizungumza na wanahabari jijini Mbeya baada ya kukamilika kwa mkutano uliowakutanisha viongozi wa makanisa mbalimbali utakaotekelezwa katika wilaya ya Kilwa kwa ufadhili kutoka serikali ya Israel.

Askofu Prof. Silivesta Gamanywa ambaye ni Mwenyekiti wa mradi (Picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Askofu Gamanywa

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Maprofesa na Madaktari wa Teolojia Tanzania Prof. Rejoice Ndalima amesema katika kipindi hiki cha ukuaji wa teknojia ya kilimo ni vema watu kujiwekeza katika kilimo cha kisasa cha ufuta.

Prof. Rejoice Ndalima (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Maprofesa na Madaktari wa Teolojia Tanzania (Picha na Ezra Mwilwa)

Askofu Gamanywa ameongeza kuwa kanisa linaanzisha mradi huo kwa kuzingatia soko kubwa la ufuta duniani.