Baraka FM

Tulia traditional dances festival yafana Mbeya

29 September 2023, 10:46

Baadhi ya wacheza ngoma katika tamasha la Mbeya Tulia traditional dances festival (picha na Ezra Mwilwa)

Mziki ni sehemu ya maisha maisha ya binadamu,jamii inasisitizqwa kuenzi na kufuatilia mziki wa asili ili kudumisha mila,destri na tamaduni

Na Ezra Mwilwa

Mstahiki meya wa jiji wa Mbeya Dormohamed Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Mbeya kuyatumia maonesho ya ngoma za asili kupata fursa ili kujiinua kiuchumi.

Ameyasema hayo wakati akifungua maonyesho ya ngoma za asili mkoa wa Mbeya yaliyofunguliwa rasmi leo katika viwanja vya airpot ya zamani jijini Mbeya. 

Mstahiki meya wa jiji wa Mbeya Dormohamed Issa(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Mstahiki meya wa jiji wa Mbeya Dormohamed Issa

Mwenyekiti wa maandalizi ya maonyesho hayo Adam Mwakatumbula amesema wanamshukuru dk. Tulia Akson kwa kuanzisha tamasha hilo ambalo linawaunganisha watu mbalimbali na kudumisha umoja wa kitaifa.

Mwenyekiti wa maandalizi ya maonyesho Adam Mwakatumbula(picha na Ezra Mwilwa)
sauti ya mwenyekiti wa maandalizi ya maonyesho Adam Mwakatumbula

Aidha katibu wa machifu mkoa wa mbeya Ilanga Mwanamtwa amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa amani hivyo watu wote wanakabishwa kushiriki.

Sauti katibu wa machifu mkoa wa mbeya Ilanga Mwanamtwa

Diwani wa kata ya Iyela Mussa Ismail amesema kufanyika kwa tamasha hilo katika kata yake kunasaidia kuinua uchumi wa kata  yake.

Diwani wa kata ya Iyela jijini Mbeya Mussa Ismail(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Diwani wa kata ya Iyela jijini Mbeya Mussa Ismail