Baraka FM

Akutwa na nyaraka za serikali na meno ya trmbo Songwe

6 February 2024, 11:17

Na mwandishi wetu, Songwe

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa kuishirikisha jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kufanya doria, misako na operesheni ambapo limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa 01 kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali Meno 09 ya Tembo yenye uzito wa Kilogramu 20 bila kuwa na kibali.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Gallus Hyera ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia Mtuhumiwa 01 mwenye umri wa miaka (52) mkazi wa Msia kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali meno ya tembo.

Mtuhumiwa alikamatwa Januari 30, 2024 katika msako uliofanywa katika Kijiji cha Ibembwa kilichopo Kata ya Igamba, Wilayani Mbozi akiwa ameficha meno ya tembo kwenye Begi aliloliweka ndani ya mfuko wa Sandarusi akiwa kwenye harakati za kutafuta wateja.Aidha katika upelelezi wa awali umebaini kuwa Mtuhumiwa ni muwindandaji haramu,msafirishaji na muuzaji wa nyara za serikali, atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe ambao wanajihusisha na uhalifu wa nyara za serikali kuacha mara moja kwani awatoweza kukwepa mkono wa sheria.