Baraka FM

Kanisa la Moravian Tanzania kupata maaskofu wawili 2023

24 October 2023, 15:54

Kanisa la Moravian kupitia taratibu zake linatarajia kupata maaskofu wawili ili kuendeleza huduma za kiroho katika dhehebu hilo.

Na Deus Mellah

Wakristo wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi na jimbo la kaskazini wametakiwa kuendelea kumuomba Mungu ili waweze kuchagua maaskofu watakao waongoza kiroho,kimwili na kiuchumi.

Wito huo umetolewa na katibu wa idara ya maandiko wa kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kaskazini Mch. Dr. Ipyana Mwangota wakati akizungumza na kituo hiki kuhusu wakristo kuendelea kuombea uchaguzi wa Askofu wa jimbo la Kusini Magharibi na jimbo la Kaskazini

Mch. Dr. Ipyana Mwangota katibu wa idara ya maandiko wa kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kaskazini (picha na Deus Mellah)
sauti ya katibu wa idara ya maandiko wa kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kaskazini Mch. Dr. Ipyana Mwangota

Naye mch Ibrahim Nzowa wa kanisa la Moraviani jimbo la kaskazini  ushirika wa Nkuhungu Dodoma   amewaomba wachungaji na wajumbe kuhakikisha wanaendelea kumtegemea Mungu pekee katika uchaguzi huo.

Mch Ibrahim Nzowa wa kanisa la Moraviani jimbo la kaskazini  ushirika wa Nkuhungu Dodoma (picha na Deus Mellah)
Sauti ya Mch Ibrahim Nzowa wa kanisa la Moraviani jimbo la kaskazini  ushirika wa Nkuhungu Dodoma

Mmoja wa wakristo wa kanisa hilo Ibrahimu Mwankitu amewashukuru viongozi wa jimbo kwa kuendelea kutoa elimu kuhusu ushiriki wa kuchagua viongozi wenye wito wa kuongoza kanisa.

Waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Nkuhungu Dodoma wakifuatilia ibada (picha na Deus Mellah)
Sauti ya muumini wa kanisa la Moravian Nkuhungu dodoma Ibrahimu Mwankitu

Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa Askofu wa kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi utafanyika novemba 2 wakati jimbo la kaskazini itakuwa novemba 15 hadi 18 mwaka huu.