Baraka FM

Mawakala ununuzi wa pareto wapigwa msasa

12 May 2026, 08:07

Baadhi ya mawakala wa ununuzi wa pareto kutoka kampuni ya PCT (picha na Ezra Mwilwa)

kufuatia changamoto ya utoroshaji wa zao la pareto kwa baadhi ya watu wanao daiwa kuwa mawakala serikali imejipanga kudhibiti changamoto hiyo.

Na Ezra Mwilwa

Mawakala wa ununuzi wa zao la pareto wametakiwa kuzingatia taratibu na njia bora za ununuzi wa zao hilo, pamoja na kutumia mizani iliyokaguliwa rasmi ili kuhakikisha haki na uwazi kwa wakulima.

Mawakala wa ununuzi wa pareto wakipatiwa elimu mbalimbli (picha na Ezra Mwilwa)

Wito huo umetolewa afisa kilimo wa wilaya za Mbeya Cathibeti Mwinuka amesisitiza umuhimu wa kufuata sheria na kanuni za ununuzi wa mazao ili kulinda maslahi ya wakulima na kuongeza ufanisi katika biashara ya pareto.

Naye Rachel Ndaro kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Uyole (TARI Uyole)amesema kwa sasa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa mbegu rasmi za zao la pareto, huku akibainisha kuwa watafiti wapo katika hatua za mwisho za kupata mbegu bora na rasmi zitakazosaidia kuongeza uzalishaji na ubora wa zao hilo.

Baadhi ya mawakala wa kambuni ya PCT(picha na Ezra Mwilwa)

Aidha viongozi wa kampuni ya PCT Edesius Mbegu pamoja na Misa Malubalo, wameeleza changamoto mbalimbali zinazoikabili kampuni hiyo katika shughuli za ununuzi huku wakieleza matarajio yao ya kuboresha huduma na kuongeza mafanikio katika msimu ujao.