Baraka FM

Sekondari Onicah watoa msaada wa lishe hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya

13 November 2023, 18:24

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Onicah iliyopo Mbalizi wakigawa misaada kwa wazazi wa watoto(picha Yudah Jay)

Na Yudah Jay

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Onicah iliyopo Mbalizi wametoa msaada wa vyakula lishe kwa baadhi ya watoto wagonjwa wa utapiamlo waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Watoto kanda ya Mbeya.

Wakizungumzana na kituo hiki wanafunzi hao wamesema misaada hiyo itawasaidia watoto waliolazwa kwa changamoto hiyo na hatimaye waweze kutimiza malengo yao baada ya kupona.

Sauti za baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Onicah iliyopo Mbalizi

Akikabidhi msaada huo Mwalimu Joshua Kandonga amesema pamoja na umri wa wanafunzi wake kuwa mdogo ila wameungana pamoja na kutoa msaada huo.

Sauti ya Mwalimu Joshua Kandonga

Akipokea msaada huo muuguzi wa zamu Jonathan Jonathan amesema ugonjwa wa utapiamlo unasababishwa na mtu kukosa vyakula vyenye virutubishi hivyo msaada huo utawasaida watoto wanaougua utapiamlo.

Sauti ya muuguzi wa zamu Jonathan Jonathan

Baadhi ya wazazi wa watoto waliopokea msaada wamesema muda mwingi wanashinda hospitalini hivyo muda mwingi wanashindwa kuingiza kipato na kusababisha kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Sauti ya Baadhi ya wazazi wa watoto waliopokea msaada