Baraka FM

Miundombinu mibovu sekondari Ruiwa chanzo cha kushuka ufaulu

13 October 2023, 19:31

Miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wengi ni pamoja na miundombinu ya vyumba vya madarasa hivyo wadau wanaombwa kutatua changamoto za wanafunzi wanazokumbana nazo.

Na Ezra Mwilwa

Ubovu wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Ruiwa iliyopo halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya unatajwa kuwa chanzo cha kurudisha nyuma taaluma za wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Hayo yamezungumzwa na mkuu wa shule hiyo Reni Ngenzi wakati akisoma risala katika mahafali ya wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza kidato cha nne mwaka 2023 shuleni hapo.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ruiwa Mbarali Mbeya akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha nne(picha na Ezra Mwilwa)

Sauti ya mkuu wa shule Reni Ngenzi wakati akisoma risala katika mahafari ya wanafunzi

Kwa upande wake diwani wa kata ya Maongole Patric Mwisoba amesema shule ya Ruiwa hivi sasa imebaki ikihudumia wanafunzi kutoka kata moja tofauti na awali ilipokuwa ikihudumia zaidi ya kata moja.

Sauti ya Diwani wa kata ya Maongole Patric Mwisoba

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Sara Mwangasa baada ya kusikia changamoto zote shuleni hapo amefanikiwa kuchangisha zaidi ya sh.milioni mbili ili kusaidia uboreshwaji wa miundombinu ya madarasa na upatikanaji wa maji.

Mgeni rasmi katika mahafali Sara Mwangasa(aliyevaa skafu)akiwa na viongozi baadhi wa shule(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Mgeni Rasmi katika mahafali Sara Mwangasa