Baraka FM

Kada CHADEMA alia na serikali ugumu wa maisha

26 September 2023, 12:15

Kada wa CHADEMA David John Mwambigija (Picha na Josea Sinkala)

CHADEMA kata ya Kandete Busokelo kinafanya mkutano huo ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe na safu yake wanaotarajiwa kuwa na mikutano katika wilaya ya Rungwe.

Na Josea Sinkala

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kata ya Kandete Busokelo wilayani Rungwe kimefanya mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa ni David Mwambigija aliyeeleza serikali kupoteza dira na nia ya kweli kuwaletea maendeleo wananchi.

Akizungumza kwenye mkutano huo, aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Mbeya Mjini David John Mwambigija amelia na serikali kuwa chanzo cha hali ngumu ya maisha na kwamba imeshindwa kusimamia rasilimali za taifa ikiwemo bandari ambayo imegomewa na wananchi wengi hapa nchini.

Mwambigija amesema anaishangaa serikali na kuwashauri viongozi kujitafakari kwa utendaji kazi wao hasa kuwafuatilia washauri na wakosoaji anaowaita ni wazalendo akiwemo wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi na mwimbaji Sifa Bujune wote wa mkoani Mbeya.

Kada wa CHADEMA David John Mwambigija akiendelea kuzungumza na wananchi wa Kandete Busokelo Rungwe (Picha na Josea Sinkala)
Sauti ya Kada wa CHADEMA David John Mwambigija

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Busokelo Julias Mwaipinga amewataka wanachama na wananchi kwa ujumla kushikamana kuelekea chaguzi zijazo ili kuchagua viongozi makini kupitia chama hicho akisema viongozi wa sasa wamekuwa wa maslahi yao binafsi.

Baadhi ya wanachama na wafuasi Kandete Busokelo wakicheza mziki wenye ujumbe juu ya chama chao(picha na Josea Sinkala)
Sauti ya Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Busokelo Julias Mwaipinga

Viongozi mbalimbali walioambatana na John Mwambigija kutoka Mbeya Mjini na Mbalizi wameeleza machungu wanayoyaona kwa taifa na kutoa dira ya kupata viongozi kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sauti ya baadhi ya viongozi walihudhuria mkutano

CHADEMA kikiwa na agenda mbalimbali ikiwemo +255 Katiba mpya na okoa Bandari zetu ambayo Mwenyekiti Mbowe anaendelea kuzunguka nchini kuisemea wakionyesha kutokubaliana na mkataba wa bandari kati ya Tanzania na kampuni ya Dp World ya Dubai na kutoa elimu na haja ya kupatikana kwa Katiba mpya.

Baadhi ya wananchi na wafuasi wa CHADEMA wakiwa wanafuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea katika mkutano eneo la Kandete Busokelo(picha na Josea Sinkala)