Baraka FM

Jeshi la polisi Mbeya latakiwa kufanya kazi kwa weledi

13 February 2024, 08:38

Na Hobokela Lwinga

Jeshi la polisi mkoani Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kumtanguliza Mungu ili kufikia malengo ya jeshi na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi SACP Robert Mkisi amewaasa alipotembelea Mkoa wa Mbeya na kukutana na mwenyeji wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga na Maafisa wengine na kufanya mazungumzo.

Mkisi alipata kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi ikiwemo Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania zamani CCP, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma.