Baraka FM

Kanisa kushirikiana na serikali kutoa elimu ya vyuo,kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana

9 December 2023, 09:34

Wanafunzi wahitimu chuo cha ufundi stadi cha ilindi wakiwa katika mahafali chuoni hapo (picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi limesema nia yake ni kuiunga Serikali katika utoaji wa huduma bora hasa katika sekta ya elimu.

Hayo yamesemwa na askofu mteule na mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani katika mahafali ya chuo Cha ufundi stadi cha Ilindi kilichopo kata ya Isuto halmashauri ya wilaya ya Mbeya kinachomiliki na kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi.

Mchungaji Pangani amewataka wazazi kutumia fursa ya kuwapeleka watoto wao kusoma chuoni hapo kuliko kuwaacha watoto kulanda landa mitaani.

Askofu mteule na mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya askofu mteule na mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani

Aidha mchungaji Pangani amewataka vijana hao wahitimu kwenda kuwa waaminifu na waadilifu kwenye jamii wanayokwenda kuitumikia.

Nae kaimu afisa mtendaji wa kata ya Isuto Saimon Msokwa amesema wao kama serikali watahakikisha vijana wote wenye sifa ya kujiunga na vyuo au shule wanakwenda kusoma na mzazi atakae kaidi atachukuliwa hatua za kisheria.

kaimu afisa mtendaji wa kata ya Isuto Saimon Msokwa(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya kaimu afisa mtendaji wa kata ya Isuto Saimon Msokwa

Hata hivyo mkuu wa chuo cha Ilindi Fatuma Mwaigaga amesema chuo hicho kimekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga mbalimbali tangu kilipo anzishwa.

Mkuu wa chuo cha Ilindi Fatuma Mwaigaga (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mkuu wa chuo cha Ilindi Fatuma Mwaigaga

kwa upande wake mkurugenzi wa mipango na maendeleo ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ndugu Essau Swillah ameshukru kwa ushirikiano wanaoupata kwa jamii katika utekelezaji wa utoaji wa elimu.

Mkurugenzi wa mipango na maendeleo ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ndugu Essau Swillah(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mkurugenzi wa mipango na maendeleo ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ndugu Essau Swillah

Baadhi ya wazazi wa wahitimu katika chuo hicho wamesema kanisa la Moravian limekuwa na utaratibu mzuri wa kujali jamii hivyo wameomba liendeee na mfumo huo.

Sauti za baadhi ya wazazi wa wahitimu

chuo cha ufundi stadi cha Ilindi kilianzishwa na Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mwaka 2016 na katika mahafali hiyo kwa mwaka 2023 wanafunzi 18 wamehitimu fani ya ushonaji.