Baraka FM

Makonda aweka jiwe la msingi madarasa shule ya sekondari Ivumwe

8 February 2024, 15:49

Na Hobokela Lwinga

Mapema asubuhi ya leo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu.

Paul Makonda ameweka jiwe la msingi katika muendelezo wa ujenzi wa Madarasa katika shule ya Sekondari ya Ivumwe.

Shule hiyo inatokana na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi katika kuhakikisha watoto wanaendelea kupata elimu wakiwa katika madarasa mazuri na yenye kukidhi mahitaji.

Mwenezi Makonda ametoa pongezi kwa Jumuiya ya Wazazi Taifa kwa kuendelea kuboresha na kurudisha jukumu lao ambalo ni wajibu wa Jumuiya hiyo.

Makonda ametoa rai kwa Wazazi kuendelea kutambua wajibu wao wa walezi wa jamii.

“Nitoe rai kwa Jumuiya ya Wazazi, hiki mnachokifanya ni jambo jema sana na la kupongezwa, endeleeni kutambua wajibu wenu wa walezi katika jamii kwakuwa ndio ujenzi wa kesho njema ya Nchi yetu””Yatupasa kujua kwamba wanachopambania Jumuiya ya Wazazi si kwa watoto hawa pekee bali ni kwa Taifa letu kwa ujumla katika kizazi cha siku za mbeleni”.

Aidha, Makonda baada ya kupokea changamoto ya maabara katika shule hiyo, ametoa ahadi kama idara ya uenezi ya Chama Cha Mapinduzi nayo itaunga mkono katika kuwezesha shule hiyo.