Baraka FM

Fahamu jinsi mifumo ya maisha inavyosababisha ongezeko la magonjwa

11 September 2023, 12:49

Sehemu ya eneo la Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Picha na mtandao

Katika maisha ya binadamu kumekuwa na mifumo mbalimbali ya maisha, ambapo watanzania walio wengi wana tabia ya kutozingatia afya hasa katika suala la ulaji hali inayowafanya wakumbwe na magonjwa mbalimbali.

Na Hobokela lwinga

Kutokana na mifumo mbalimbali ya maisha kuchangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, jamii imetakiwa kuzingatia kwenda mara kwa mara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata vipimo vitakavyowafanya kufahamu hali ya afya zao.

Wito huo umetolewa na daktari bingwa wa magonjwa sugu yasiyo ya kuambukizwa kutoka hospitali ya rufaa Kanda ya Mbeya Dkt. Joyce Komba wakati akizungumza na kituo hiki mapema leo kuhusiana na ugonjwa wa kisukari.

Dkt. Komba amesema takwimu zinaonesha kuwa wanaume ndio wanakumbwa zaidi na ugonjwa huo kuliko wanawake.

Sauti ya Dkt. Joyce Komba

Aidha Dkt. Komba amesema sababu kubwa ya mtu kupata ugonjwa wa kisukari ni mtu kushindwa kula chakula kwa wakati na kwa kuzingatia mlo kamili.

Sauti ya Dkt. Joyce Komba

Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya wamesema hawana uelewa wowote juu ya ugonjwa wa kisukari hivyo wameziomba mamlaka zinazohusika kuongeza juhudi ya utoaji wa elimu.

Sauti za wananchi mkoa wa Mbeya

Katika maisha ya kila siku  ili mtu aweze kuepukana na magonjwa  yasiyo ya kuambukizwa  hana budi kuzingatia ufanyaji wa mazoezi ya mwili kila siku.