Baraka FM

Walimu Songwe DC wapewa mafunzo mtaala ulioboreshwa

11 January 2024, 11:50

Na mwandishi wetu, Songwe

Walimu kutoka Kata za Saza, Mkwajuni na Mwambani Wilayani Songwe wamepewa mafunzo ya mtaala ulioboreshwa yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mkwajuni.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Wilaya ya Songwe, Mwalimu Bunka Mtogolo amesema kuwa tayari walimu wa kata 12 wameshapata mafunzo hayo na kata zingine sita zinatarajia kuhitimisha Januari 11, 2024.

“Tunatakiwa tuzingatie mafunzo haya ili tutoke na ujuzi wa kufundisha mtaala ulioboresha. Tuyashike mafunzo haya na tukayafanyie kazi” amesisitiza Mkuu huyo wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Wilaya ya Songwe wakati akizungumza na walimu hao.

Mwalimu Bunka amewataka walimu hao kuzingatia mafunzo hayo ili mtaala huo ulioboreshwa uanze kufundishwa huku akiwasisitiza walimu hao kusimamia uboreshaji