Baraka FM

Rungwe yafanya tathmini ya matokeo ya mitihani ya taifa 2023

6 February 2024, 10:54

Na mwandishi wetu

Tathmini ya matokeo ya Mtihani wa taifa kidato cha pili na nne kwa mwaka 2023 imefanyika leo tarehe 2.2.2024 uliwakutanisha Viongozi kutoka idara ya elimu, wakuu wa shule za sekondari 45 Maafisa elimu kata kutoka katika kata 29.

Lengo likiwa ni kupata mwelekeo sahihi kuhakikisha Halmashauri inafanya vizuri zaidi katika mwaka 2024 kwa kufaulisha kwa asilimia 100% pamoja na kushika namba ya kwanza katika mkoa wa Mbeya

Kwa miaka mingi mfululizo Rungwe imekuwa ikishika nafasi ya pili katika matokeo ya kitaifa (Kimkoa) baada ya Halmashauri ya jiji la Mbeya

Msimu huu Rungwe inanyemelea nafasi ya kwanza kutokana na kuwa na mikakati madhubuti ya ufundishaji, upatikanaji wa chakula cha mchana kwa walimu na wanafunzi, uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia, udhibiti wa nidhamu mbaya kwa wanafunzi pamoja na upatikanaji wa vitabu shuleni.

Katika matokeo haya Kwa mtihani wa upimaji kidato cha pili (FTNA) Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imefaulisha mpaka kufikia asilimia 91% huku shule za serikali kama KAYUKI, TUKUYU, BULYAGA, KIWIRA NA KINYALA zikifanya vizuri. Shule binafsi zilizofanya vizuri ni pamoja na JOY GIRLS, ST. ALMANO, GOD’S BRIDGE, LUBALA, GREEN WOOD NA NDEMBELA.

Kwa upande wa mtihani wa kidato cha nne (CSEE) Halmashauri imefaulisha kwa asilimia 95.9% Huku shule za serikali zilizofanya vizuri zikiwa ni pamoja na KAYUKI, TUKUYU, KIWIRA, BULYAGA , NDEMBELA ONE. Shule binafsi zilizofanya vizuri ni ST.ALMANO, GOD’S BRIDGE, KIPOKE, NDEMBELA, LUTENGANO NA MPOROTO.