Baraka FM

Katibu Mkuu Moravian Mwakilasa,Vijana acheni anasa mtumikeni Mungu

10 October 2023, 07:06

Vijana wakiwa katika ibada ya mkutano wa vijana katika kanisa la Moravian Mswiswi Mbarali Mbeya (Picha na Hobokela Lwinga)

Ili kuhakikisha jamii inakuwa na kizazi kilicho bora kuna kuwa hakuna budi kuanza kuwajenga vijana kulingana na rika zao,kanisa la Moravian limekuwa na utaratibu mzuri wa kuwakutanisha vijana kutoka shirika zake mbalimbali lengo likiwa ni kujipa tathini ya mwenendo wa kujenga maadili ya ndani na nje ya kanisa.

Na Hobokela Lwinga

Vijana wa kikristo nchini wametakiwa kujitoa kwa moyo kufanya kazi ya Mungu kutokana na kiwango cha imani yao kwa Mungu ili kuhakikisha ulimwengu unahubiriwa habari njema.

Wito huo umetolewa na katibu mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ndugu Israel Mwalukasa katika mkutano wa vijana kati wa kanisa hilo uliohitimishwa katika ushirika wa mswiswi uliopo katika halmashauri ya wilaya ya mbarali.

Ndugu Mwalukasa amewapongeza vijana hao kwa kushiriki mkutano huo huku akisema mkutano huo unautofauti na mikutano mingine kwani mwaka huu mpaka wachungaji wameshiriki kuonyesha fani zao kwa kuimba.

Katibu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi Ndugu Israel Mwakilasa akizungumza na vijana katika ushirika wa Mswiswi Mbarali Mbeya(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya katibu mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ndugu Israel Mwalukasa

Akihubiri katika ibada ya kuhitimisha mkutano,katibu wa idara ya vijana kutoka jimbo la kusini rungwe much.dastan mwasomola amesema vijana wa Kanisa wanapaswa kuwa kielelezo na kuachana na mambo maovu ili kuujenga mwili wa kristo na kanisa kwa ujumla. 

Katibu wa idara ya vijana jimbo la kusini akihubiri katika mkutano wa vijana Mswiswi Mbarali Mbeya(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya katibu wa idara ya vijana kutoka jimbo la kusini rungwe much.dastan mwasomola

Hata hivyo mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya mbarali mch.Amosi mwampamba amewashukru washiriki kwa kujitoa kushiriki mkutano huo na kuacha shughuli zao za kila siku.

Sauti ya mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya mbarali mch.Amosi mwampamba

Mkutano huo wa Kanisa umejumuisha vijana wa Jimbo zima kutoka katika wilaya mbalimbali za kanisa ikiwemo wilaya ya Mbeya, chunya,mbalizi na mbarali.