Baraka FM

Wazazi na walezi msiwaachie walimu watoto wenu

19 October 2023, 18:39

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya akitoa maelekezo kwa mwanafunzi wa shule ya msingi mtumbo(picha na Daniel Simelta)

Hivi karibu kumekuwa masuala ya kikatili ambayo yamekuwa Yakifanywa kwa wanafunzi na walimu wao,kitendo hicho kimekuwa kikwazo na kuondoa iman ya kuwaamini baadhi ya walimu.

Na Daniel Simelta

Wazazi na Walezi mkoani Songwe, wametakiwa kuimarisha malezi kwa watoto wao na sio kuwaachia walimu jukumu hilo.

Akizungumza wakati akitoa elimu ya Ushirikishwaji Jamii kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mtumbo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya, amesema endapo malezi ya watoto yataimarishwa na kusimamiwa vyema ni wazi kuwa hakutakuwa na mmomonyoko wa maadili utakaochangia watoto kutofikia malengo yao kielimu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya akiendelea kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi mtumbo(picha na Daniel Simelta)

Sanjali na hayo Kamanda Mallya amesema ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ni lazima kuimarisha malezi bora kwa watoto wetu ikiwa ni pamoja na kufuatilia mabadiliko ya tabia zao.

Kwa upande wa walimu wa shule hiyo mbali ya kupongeza jitihada mbalimbali za Jeshi la Polisi katika kuyafikia makundi yote kwenye jamii waliahidi kuwafikishia ujumbe huo wazazi wa wanafunzi kupitia vikao vya wazazi shuleni hapo.

wanafunzi wakimsikiliza Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya (picha na Daniel Simelta)