Baraka FM

Wakristo onesheni upendo kwa watu wote

1 April 2024, 19:25

Mchungaji Moravian ushirika wa Mswiswi Shadrack Kayange (picha na Deus Mellah)

Upendo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kila mtu anapaswa kuonesha upendo pasipo kujali rika rangi wala kabila.

Na Deus Mellah

Wakristo wa madhehebu mbalimbali mkoani Mbeya wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuonesha upendo kwa watu wa makundi mbalimbali katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mch Joram Mwaisumbe wakati wa ibada ya pasaka iliyofanyika katika kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi ushirika wa Mswiswi wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Mch Joram Mwaisumbe Amesema ili mkristo ni kielelezo katikajamii hivyo ni wajibu wao kuonesha upendo kwa watu wa rika mbalimbali.

Mch Joram Mwaisumbe akihubiri Moravian katika Ibada ya Pasaka Moravian Mswiswi (picha na Deus Mellah)

Naye Mchungaji Moravian ushirika wa Mswiswi Shadrack Kayange amesema kuwa ni vyema wakristo wakaendelea kuonesha upendo kama Yesu Kristo alivyokuwa anaonesha upendo kwa watu wote.