Baraka FM

Mkoa wa Songwe watoa msaada kwa  waathirika wa mafuriko Hanang’ 

12 December 2023, 18:38

 Na Mwandishi Wetu,Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt Francis K. Michael, amepokea msaada kutoka kwenye Kikundi cha Tunduma ni Fursa Online 11 Desema 2023. ambacho kimetoa tani moja ya mahindi, kilo 250 za sabuni, mavazi pamoja na viatu kwa ajili ya msaada kwa waathirika wa mafuriko katika wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.

Akizungumza nje ya ofisi yake wakati wa kupokea msaada huo, Mhe. Dkt Francis amewashukuru wana Tunduma hao kwa kujitoa kuunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia utatuzi wa adha zinazowakabili wananchi waliokumbwa na maafa mkoani Manyara.

Pamoja na kuwashukuru watu hao, Mkuu wa Mkoa amewaomba wadau wengine kuendelea kuungana na serikali ambayo kwa kipindi hiki ambacho nguvu kubwa hasa ya kiuchumi imeelekezwa huko (Hanang’) ili kurejesha hali ya kawaida kwa wananchi walioathirika.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt Francis K. Michael akipokea msaada kutoka kutoka kwenye Kikundi cha Tunduma ni Fursa Online(Picha na mwandishi wetu)

Mwenyekiti wa Kikundi cha Tunduma ni fursa Online amesema wamehamasika kuchangisha na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo Vyakul, sabuni na mavazi kuitikia kwa vitendo ombi la Serikali kuwaomba wadau na taasisi mbalimbali kutoa michango kwenye Wilaya na Mikoa mbalimbali kupitia wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya.