Baraka FM

Askofu Mwakanani apata mchumba,kufunga ndoa mwakani 2024

31 October 2023, 09:06

Askofu Rabi Mwakanani akiwa amemvisha Pete ya uchumba wakili msomi bi.Sylivia Elia(picha na Kelvin Lameck)

Mungu aliona si vyema mwanaume akawa peke yake akamfanyia msaidizi,hivyo ndoa ni mpango wa Mungu na ndio maana Mithali 18:22 inasema Apataye mke apata kitu chema;Naye ajipatia kibali kwa BWANA.

Na Kelvin Lameck

Askofu wa makanisa ya Evangelical Brotherhood Tanzania Rabi Mwakanani ametangaza uchumba na bi.Sylvia Elia ambaye ni wakili msomi.

Askofu amechukua maamzi hayo baada ya kufiwa na mke wake takribani miaka mitatu iliyopita na tukio hilo limefanyika katika kanisa la Evangelical Brotherhood ushirika wa Mbeya mjini.

Hata hivyo askofu Mwakanani anatarajia kufunga ndoa mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2024, hivyo katika Safari hii kila mmoja mwenye mapenzi mema anawajibu wa kuombea ratiba hii.

Huyu ndiye mchumba wa askofu Rabi Mwakanani wakili msomi Bi.Sylvia Elia(picha na Kelvin Lameck)

Askofu Mwakanani ni miongoni mwa watumishi wa Mungu wanaofanya kazi ya kuhubiri,kufundishaa na kuomba na wasikilizaji wa kituo cha radio Baraka cha jijini Mbeya.