Baraka FM

Wakaguzi, askari Njombe wapongezwa kupitia sifa, zawadi

26 June 2024, 13:21

Hawa ni sehemu ya wakaguzi na askari waliopongezwa kutokana na utendaji wao wa kazi (Picha na mwandishi wetu)

Uadilifu mahala pa kazi ni moja ya nyenzo ambayo inampa nafasi mfanyakazi kuaminiwa na watu wanaomzunguka mtu, katika hali inamfanya mtu kupendwa na wakati mwingine kupongezwa

Na Mwandishi Wetu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Hassan Banga Juni 26,2024 ametoa zawadi kwa wakaguzi na askari waliofanya vizuri mkoa wa Njombe.

Kamanda banga, amewapongeza wakaguzi hao na askari kwa kufanya kazi zao wa weledi na uadilifu mkubwa na kuwataka kuendelea kuzingatia maadili kama kauli mbiu ya Jeshi la Polisi inavyotutaka ya nidhamu, haki ,weledi na uadilifu kama chachu ya kuendelea kufanya vizuri katika utendaji wa kazi.

Pia, zawadi hizo zimetolewa wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wapatao 7 kutoka vitengo mbalimbali kwa niaba ya Mkuu Jeshi la Polisi Tanzania afande IGP Camillius Wambura.

Aidha ,Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa na utaratibu wa kuwapongeza askari wanaofanya vizuri ili kuongeza ufanisi na uadilifu katika utendaji wa kupitia sifa na zawadi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Hassan Banga(picha na mwandishi wetu)