Baraka FM

Mkuu wa mkoa wa Songwe aridhishwa na hatua za ujenzi wa wa shule mpya ya Izuba

9 January 2024, 18:49

Na Mwandishi wetu,Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt. Francis K. Michael, amekagua ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Izuba Kata ya Isongole Wilayani Ileje na kueleza kuridhishwa na mwenendo wa ujenzi shule hiyo.

Mkoa wa Songwe amefanya ukaguzi huo na kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi kwa usimamizi mzuri wa mradi huo wa maendeleo kupitia Sekta ya Elimu ambapo pia ameshiriki zoezi la upandaji miti katika shule hiyo mpya.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi amesema katika kupambana na utunzaji mazingira Wilaya yake imeanza kutekeleza maelekezo ya Mkoa ya kuhakikisha kila Halmashauri inapanda miche ya miti million mbili.