Baraka FM

Zimamoto Mbeya yatoa elimu shule za msingi

5 October 2023, 22:06

Afisa habari wa Zimamoto na Uokoaji mkoani Mbeya Copl. Ester Kinyaga akitoa elimu kwa wanafunzi. (Picha na Mwandishi wetu)

Elimu ni msingi wa maendeleo, kila mtu anapaswa kupata elimu ili kuweza kufanikiwa juu ya jambo ambalo anatamani kulijua haijalishi umri, hapa jeshi la zimamoto linaonesha wazi namna ambavyo limeendelea kutoa elimu ili kuwezesha wananchi kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo moto.

Na Mwandishi wetu

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mbeya limetoa elimu ya kukabiliana na majanga mbalimbali shule ya msingi Mkapa jijini Mbeya.

akizungumza katika shule ya Mkapa English Medium, afisa habari wa jeshi hilo mkoa wa Mbeya Copl. Ester Kinyaga amesema lengo ni kuwajengea uwezo wanafunzi hao kujifunza namna ya kukabiliana na majanga ya moto kwenye maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Copl. Ester Kinyaga akiendelea na utoaji wa elimu ya zimamoto na uokoaji shule ya msingi Mkapa (Picha na mwandishi wetu)

Copl. Kinyaga amesema jeshi lake lina wajibu wa kutoa elimu kwa mwananchi yeyote pasipo kubagua rika, rangi, dini, kabila wala maumbile.

Aidha ameendelea kusisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa wakati pindi wanapokumbana na ajali za moto ili kuweza kupata huduma kwa haraka kutoka kwa jeshi hilo.

Mmoja ya wanafunzi shule ya msingi Mkapa jijini Mbeya akifuatilia jarida lenye maelezo ya namna ya kufikisha taarifa jeshi la zimamoto (Picha na mwandishi wetu)
Sauti ya afisa habari wa zimamoto na uokoaji Mbeya Copl. Ester Kinyaga