Baraka FM

RPC Mbeya awataka wanafunzi kuacha uharifu

26 October 2023, 16:06

kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin kuzaga(picha na Hobokela Lwinga)

Katika kupambana na ugarifu elimu inapaswa kuanzia chini ya ngazi ya familia hasa kwa watoto ,mkoa wa mbeya kupitia jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kupitia shule mbalimbali ili kukabiliana na matukio ya kiharifu ikiwemo ukatili wa kijinsia.

Na Hobokela Lwinga

Jeshi la polisi mkoani mbeya limewataka wanafunzi wa shule mbalimbali kusoma kwa bidii badala ya kujiunga na makundi yasiyofaa.

Hayo yameelezwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin kuzaga akiwa na mkuu wa dawati la jinsia na watoto Lovenes Mtemi wakati wa ziara katika shule ya msingi azimio iliyokuwa na lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la nne kuhusiana na masuala ya ulinzi na usalama.

kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin kuzagaakifurahia jambo na mwanafunzi(picha na Hobokela Lwinga)
sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin

Akizungumza na wanafunzi hao, kamanda Kuzaga amewataka kujiepusha na makundi yasiyofaa na badala yake wajikite katika masomo kwa kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kufaulu.

Aidha, kamanda Kuzaga amewataka wanafunzi hao kutokaa kimya dhidi ya vitendo vya uhalifu na kuwasisitiza kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu kwa walimu, wazazi na jeshi la polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

Wanafunzi wa shule ya msingi Azimio jijini Mbeya wakimsikiliza RPC mkoa wa mbeya(picha na Hobokela Lwinga)